kwanza napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa MUNGU mwenyezi kwa kunipa ngvuvu afya, akili na uwezo kwa kupenda kujifunza na kutambua yanayoendelea duniani siku hadi siku. Ama kwa hakika ninakiri ya kwamba kuwepo kwetu hapa duniani kuna sababu zake.
Pia napenda kuwashukuru wana globu wengine ambao wamekwisha tangulia, kipekee nimshukuru kwa ndugu Deus Gunza ambaye kwaye kupitia globu yake www.butiama.podomatic.com nimeweza kusikia mahojiano kati yake ndugu Ndesanjo Macha ambayo yamepelekea nami kuanzisha blogu hii yangu, asante sasa ndugu Macha "Gandhi" kama ulivojiita kwenye blogu yako www.jikomboe.com , uelimishaji wako umenipa nguvu ya kuanzisha blogu hii bila ya shida na wasi wasi wowote. Labda ninaahidi kuendeleza elimu hii kwa ndugu wengine duniani hasa watanzania wenzangu ambao bado tuko nyuma katika tekinolojia hizi mpya. Sababu zinaweza kuwa na hali duni ya maisha au la kasumba ya kutopenda kujifunza.
Kwangu huu ni mwanzo tu, niko mbioni kutengeza tovuti kamili na mara kwa mara nitahitaji msaada wenu ninyi mlio tutangulia katika tekinolojia hii na zaidi napenda kuchua fursa hii kuwakaribisha nyote katika blogu yangu, na kwa wale wageni au wapya katika tekinolojia hii nami najiunga na waliotangulia kusema kwamba niko tayari kushiriki katika kuelimishana.
Labda nimalizie kwa kusema, "HIZI NI ZAMA ZA HABARI" ama kweli kila mmoja wetu anaweza kuwa mwanahabari.
Manyerere, Robert! (Mwanablogu)
Monday, 18 December 2006
Subscribe to:
Posts (Atom)