Saturday, 5 May 2007
TYSCO-VIFAA VYA MICHEZO!
Viongozi wa TYSCO(Tanzania Youth Sport Charity Organisation) wamepokea msaada wa Vifaa vya michezo kama awamu ya kwanza! Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za KENT FOOTBALL ASSOCIATION katika mji wa KENT kusini mashariki mwa mji wa LONDON katika ya viongozi hao wa TYSCO Mkuregenzi Allan Kalinga,Victor Mgoya na Chief Exucutive huyo wa Kent Football Association Bwana Keith Masters.
Vifaa walivyopokea ni pamoja na Jezi tofauti tofauti yaani bukta na fulana zake, viatu jozi kadhaa, mipira zaidi ya sabini, mifuko na chupa za maji, soksi pamoja na vifaa vingine vya mazozei uwanjani! Hii ni awamu ya kwanza ya msaada huo ambapo mwishoni mwa mwezi huu wanategemea kupokea msaada mwingine ili kukamilisha ujazo wa kontena moja la futi ishirini(20ft) kabla ya kutuma vifaa hivi nchini Tanzania kwa Uanzishwaji wa matawi machache ya TYSCO ambao ufunguzi huu utahudhuriwa na Viongozi hawa wa KENT FOOTBALL ASSOCIATION na TIMU toka United Kingdom!
Endelea kutembelea blogu hii kwa habari zaidi na picha za tukio hili na mengine yanayofuata.
Ukipenda kupata habari juu ya TYSCO unaweza kuwasiliana na Allna Kalinga ama Victor Mgoya kwa simu namba +447738916447 na +441189594472.
Subscribe to:
Posts (Atom)