Friday, 11 May 2007

GGPromotion- Wedding in Reading UK!




Mkurugenzi wa GGPromotion www.geratonltd.com Gerald Lusingu ametimiza ahadi ya kuuacha ukapela kwa kufunga pingu na Bi.Sophia ambaye alimweka uchumba miezi michache iliyopita. Shughuli hii ya kupendeza iliuhudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki mbali mbali ilifanyika katika ukumbi wa RiverMade Leisure Center mjini Reading.
pata picha zaidi hapo chini!



Bwana na Bibi Harusi wakiingia ukumbini



Meza Kuu Mzee na Mama Lusingu,Balozi Mama Maajar na Mzee Sharif Maajar,Ridhiwani Kikwete, Hussein Dewji (Middle East Cargo), Abu Faraji (tzuk.net)


kwa picha zaidi tembelea tzuk.net photo gallery

Thursday, 10 May 2007

CCM LONDON CHAPTER- OFISI!


Tawi la CCM London, limepata ofisi jijini London! Ofisi hii iko mashariki mwa jiji la London na anuani ni 213 High Street North, East Ham, E6 1JG.
Jumamosi ya tarehe 12 Mei 2007 MAKAMU M/KITI CCM TAIFA, MHE. MALECELLA atatembelea ofisini hapo kusalimiana na wanachama wa CCM wanaoishi nchini Uingreza.
Habari zaidi na picha za tukio hili zitapatikana hapa.

M/Kiti wa muda wa CCM London Mh. Shaarif Maajar anawakaribisha wanaCCM wote kuja kumlaki Mh.Mallecela na kutembelea ofisi yao.

Mnakaribishwa sana!