Tuesday, 9 January 2007

GG Promotions Kuachana na Ukapela-Reading(UK)

Mkurugenzi wa kampuni ya GGPromotions www.geratonltd.com wa mjini Reading aliwaadhihirishia vijana wenzake kuwa amedhamiria kuachana na ukapela. "Engagement Party" ya Bwana Gelard Lusingu na Bi. Sophia Hayuma ilifanyika katika ukumbi wa Quality Hotel-Oxford road hapa mjini Reading j`mosi ya tarehe 6 jan 2007.


Sherehe hiyo ya kufana iliudhuriwa na wakurugenzi wa makampuni mbalimbali, wafanyabiashara binafsi na ndugu, jamaa na marafiki wasihio nchini Uingereza. Baadhi ya wakurugenzi hao ni Juma Mabakila www.goce.co.uk ,Hussein Dewji www.middleeastcargo.com , www.francophonespace.com, Abu Faraji www.tzuk.net ,Ingusi www.cemvo.org, bongoflava store na wengine wengi.

Tunawapongeza kaka Gerald na Bi Sophia kwa uamuzi mliofikia, tunasubiri mwaliko wa ndoa. MUNGU awalinde na kuwatia nguvu na ujasiri, sisi tuko pamoja nanyi.

Endelea kutembelea blogu hii kwa picha za tukio hilo.

Mwishoni mwa wiki hii tutawaletea habari za uzinduzi wa tawi la CCM mjini London na Habari za ujio wa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuonana na watanzania waishio nchini Uingereza. Watanzania waishio Uingereza wamekuwa wakisubiri kwa hamu kuonana na Rais wao mpya, je ni yapi waliyonayo kuwakilisha kwa Rais? Usikose makala hii

No comments: