Monday, 12 March 2007

CRDB BANK ABROAD- TANZANITE ACCOUNT!

Bank ya CRDB imeendelea kuijitangaza kwa kasi ya nguvu ughaibuni kupitia akaunti yake ya Tanzanite. Bank hiyo kwa kuendelea kuwatumia mawakala wake katika miji mbali mbali ya Uingereza hasa mji wa Reading na Jiji la London, imefanikiwa kupata wateja wengi zaidi kutoka United kingdom.
Mwakilishi wa CRDB bank aliyekuwapo nchini Uingereza dada Jenipher Tondi amefanikiwa kuitangaza akaunti hii ya Tanzanite kwa umakini na hivyo kupelekea vijana kwa wazee, wake kwa waume wakitanzania waishio nchini Uingereza kuonyesha kuvutiwa na huduma hiyo na kupelekea wengi wa hao kufungua akaunti hii ya Tanzanite!
Miaka miwili iliyopita benki ya CRDB ilijaribu kujitangaza nchini Uingereza lakini hii huduma ilionekana kuzorota pengine ni kwa ajili watanzania kutokueleweshwa vizuri faida za uwekezaji nchini Tanzania ama ni hali tu ya maendeleo na shinikizo na hali halisi ya maisha Ughaibuni ilivyo katika miaka hii ya karibuni.
Takwimu zinaonyesha kwamba watanzania zaidi ya elfu mbili(2000) waishio ughaibuni sasa wana akaunti ya Tanzanite. Hivi sasa huduma hii inaweza kupatikana pia kwa njia ya Internet, kama kuangalia bank statement, kulipa bills(umeme, maji, n.k) na kwamba money transfer inaweza kufanyikia kupitia baadhi ya benki kubwa za hapa nchini Uingereza kama Lloyds TSB Bank. moja kwa moja kwenye akaunti ya mteja aliye nje ya nchi bila longolongo lolote!
Kwa ufahamu zaidi unaweza kuwasiliana na dada Jenipher Tondi kwa namba +255-22-2117442/ +255-784719420 ama kwa barua pepe tanzanite@crdbbank.com ama tembelea tovuti yao ambayo ni http://www.crdbbank.com ("The Bank That Listens")

No comments: