Hivi majuzi nilipokuwa jijini Dar-es-salaam nimeshuhudia kero za foleni katika barabara zetu nyingi za hapo jijini hasa katika makutano ya barabara kuu kadha wa kadha mida ile ya kuelekea ama kutoka kazini(rush hours), ama kwa hakika kero hii si kitoto!
Jioni ya jana nimepata bahati ya kubadilishana mawazo na mdau mmoja mjasiliamali mwenzangu ambaye makazi yake yako nchini Uingereza na amejiwekea vitega uchumi kadhaa hapa UK, ameeleza kwamba hali hii ni moja ya kikwazo kikubwa katika kuwekeza nchini Tanzania. Yeye pia alikuwa nchini Tanzania kwa muda wa wiki moja hivi na amekiri kupoteza zaidi ya masaa matatu kutoka Mbezi Beach mpaka Mwenge ambapo kero hii imekuwa ikiendelea siku hadi siku.
Hivi karibuni serikali ya Tanzania imeongeza ushuru kwa Uchakavu kwa magari yanayoingizwa nchini yenye umri wa zaidi ya miaka kumi sababu moja wapo ikiwa ni kupunguza mtiririko wa magari nchini, lakini je hili ndilo soluhisho kweli la kero hii ya foleni za magari, binafsi sina hakika juu ya hilo.
Mtazamo wangu ni kwamba endapo serikali itafumbia macho urekebishwaji wa miondo mbinu (infrastructure) kwa karibu barabara zote za jijini hali itazidi kuwa ngumu siku hadi siku. Ni wazi kwamba wakati umefika sasa nasi kuwa na barabara za juu (flyovers) angalia mfano mdogo wa picha hapo juu kabisa na ring roads hasa kwenye makutano ya barabara zetu kuu kama makutano ya barabara za morogoro na mandela, pale ubungo, ama barabara za Nyerere na Kilwa pale Scandinavia(zamani KAMATA), makutanoi ya TAZARA, MNAZI MMOJA, na sehemu kadha wa kadha. Mfano mzuri nimeweza kuuona kwenye kipande cha barabara toka Mwenge mpaka Ubungo Mwisho ambayo bado ikio matengenezoni.
Sina hakika serikali/wizara husika ina mipango gani juu ya hili ila kwa kuwatumia Think Tankers wake kama wapo na watu binafsi hali inaweza kuwa nzuri. Nimeona baadhi ya mfano huku ughaibhuni baadhi ya barabara utoza ushuru kwa kila gari linalopita katika bararaba hiyo kuchangia marekebisho ya barabara husika na kama vitega uchumi na kupunguza kero pia.
Tutafika tu!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment