Sunday, 13 May 2007

Mh.Mallecella atembelea Ofisi ya CCM London



Makamu Mwenyekiti wa CHAMA CHA MAPINDUZI(BARA) Mh. Mallecella, Mb. jana alitembelea ofisi za CCM London. Hafla hii iliandaliwa na Viongozi wa Tawi pamoja na wanakamati na kuhudhuriwa na baadhi ya wanaCCM waishio nchini ingereza!



Katibu wa muda Tawi Nd.Mpopo alitoa taarifa fupi ya maendeleo ya Tawi ambapo alisema kwamba tayari Tawi hili limeshafungua shina katika Mji wa Reading na wanaangalia uwezekano wa kufanya mikutano kadhaa katika miji mingine nchini Uingereza kuendelea kuandaikisha wanachama zaidi.Naye Mh. Mallecela katika kujibu taarifa hiyo kwanza aliwapongeza vingozi hawa na kuwasisitiza wachukue muda wa kuisoma katiba ya Chama kwa Moyo. Alisema kwamba yawapasa viongozi na wanachama wake nchini Uingereza kwanza kabisa wajue dhumuni kuu la CCM ambalo ni "kuahakikisha kwamba CCM inashinda uchaguzi ujao na kutengeneza dola" na kwamba "Kiongozi wa CCM anatakiwa asiwe mtu mwenye tamaa na aeneze mtunda ya Uhuru"

No comments: