Leo tarehe 11 Agosti 2007 CHAMA CHA MAPINDUZI tawi la London wamefanikiwa kufanya mkutano wao wa kwanza katika jiji la Birmingham!
Mkutano huo ambao ulianza saa 9 hivi mchana na kumalizika saa 12 jioni kama ulivyopangwa ulionekana kuwa na mafanikio makubwa. Tofauti na mikutano kadhaa ya tawi hili ambayo imeshafanyika jijini London na katika shina la Reading, mkutano huu ulionekana kuwa na idadi kubwa zaidi ya wanawake kitu ambacho kimekuwa ni changamoto kubwa, idadi ya akina mama/dada hao ilikuwa ni zaidi ya akina mama/dada kumi na mmoja!
Baada ya M/kiti wa muda wa Tawi Ndg. Maajar Sharrif kufungua mkutano huo na kutambulisha wajumbe wa muda wa tawi na wale viongozi wa muda wa shina la Reading, wajumbe wengine na wanachama wapya nao walijtambulisha na baadhi ya wajumbe toka Reading ambao waliambata na viongozi wao wa shina nao waliweza kujitambulisha pia. Mmoja wa wajumbe toka Reading ambaye alikuwa ameambata na ubavu wake, Bwana Alan Kalinga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tanzania Youth Sports Charity Organization (TYSCO) ametimiza ahadi yake ya kujitolea kompyuta mpya kwa ajili ya ofisi ya Tawi.
Naye Katibu wa muda wa tawi ndg. Richard Mpopo alisoma historia fupi ya tawi tangu kuanzishwa mwezi wa februari 2007 na mpaka kufikia siku ya leo, ambapo aliweza kufannunu kwa kina maendelo ya tawi kwa kilichofanyika kila mwezi kuanzia tawi lilipofunguliwa, vikao vilivyokwisha fanyika, kupatikana kwa ofisi, uzinduzi wa shina la la mji wa Reading na kutembelewa na wageni ambao ni viongozi wa CCM nchini Tanzania, pia alieza malengo makuu mawili ya tawi kwa sasa ambayo ni ;
1) Kuendelea Kuandikisha wanachama wapya na
2) Kujiandaa kwa uchaguzi wa viongozi wa kudumu wa Tawi hili.
Pia mkutano huu ulifanikisha kuchagua kamati ya muda ya wana-CCM Birmingham ambao wataendeleza shughuli za chama na hatimaye kuitisha uchaguzi watakpokuwa tayari kufikia idadi ya kuweza kuunda shina lao, ambapo wasema hatawachukua zaidi ya mwezi mmoja!
Zaidi ya hapo kuliwako na vitafunwa na picha ya pamoja baada ya M/kiti kuahirisha mkutano!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment