Sunday, 18 February 2007

Mh. J.K atizimiza ahadi- London

Kama alivyoahidi hapo awali alipokutana na Watanzania waishio Uingereza mwezi wa Januari 2007, Mh. Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete, jana tarehe 17 Februari 2007 alikutana tena na wananchi wake hao kwa kipindi cha maswali na majibu. Wananchi hao ambao walikuwa wakiisubiri kwa hamu siku hii, walijitokeza kwa wingi ukumbini hapo, kwa wale waliofikiri pengine ahadi hii iliyotelewa hapo awali ilikuwa ni propaganda tu za mambo ya kisiasa, waswahili wanasema,"wameula wa chuya kwa uvivu......."

Kipindi cha maswali na majibu kilifunguliwa rasmi pale tu Mh. Rais alipokabidhiwa ukumbi na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mama Maajar, naye Mh. JK bila ya kupoteza muda alitoa ruksa kwa wantanzania kuanza kuuliza mwaswali moja kwa moja. Kwa kuwa hapakuwepo na mpango maalum wa uulizaji Mh. Rais alichukua jukumu la kuwa mwenyekiti na kuanza kupokea maswali moja kwa moja kutoka kwa wananchi wasiopungua kumi na wawili kwa mkupuo mmoja na kuyajibu moja baada ya jingine, ambapo alifanikiwa kujibu maswali yote zaidi ya ishirini na manne yaliyouulizwa na wananchi wake.

Swala ambalo tunaweza kusema lilikuwa ni gumzo ama kuchukua sehemu kubwa na majadiliano lilikuwa ni swala la Utanzania yaani uzawa ama tuseme baadhi ya wananchi wengi ambao wengine tayari wamekuwa na uraia wa Uingereza ama bado wanasubiri na hawajui hatima yao ni nini wamekuwa na hamu kubwa sana ya kujua swala la uraia wa nchi mbili limefikia wapi. Katika hao aliyekuwa kivutio zaidi cha siku ni mzee mmoja ambaye aliingia nchini katika nchi ya Malkia tangu mwaka wa 1957.

Mtazamo/ Mawazo Binafsi!
Ushauri wangu ni kwamba kutokana na hali ya maendeleo ya tekinolojia na kwamba hizi ni zama za habari(Information Age), ninafikiri kwamba Mh. Rais anapojiandaa kukutuna na watanzania wake sehemu ambazo hajatembelea ama akiwa na nafasi ya kutembelea hata zile sehemu ambazo tayari ameshazitembelea basi ujio wake unapoweka wazi siku kadhaa kabla ya uwepo wake katika maeneo husika kuwepo na mpango wa wananchi kuutuma/kuulizwa maswali au maoni yao kwa njia ya mtandao aidha barua pepe, ama tovuti maalum ili kusudi siku rasmi ya kukutana Mh. aweze kujibu tu maswali moja kwa moja kwa kwa kunukuu kutoka hizo barua pepe, hii pia itasaidia Mh. kuwa na majibu kamili na ya kiutalaamu kwa kila swali kwa maana tayari hatakuwa ameshaulizi habari(information) kamili toka kwa wizara husika au wanaohusika hivyo kurahisisha zoezi hili, kuokoa muda na kuongeza uzalishaji. Kwa muda ule mchache wa masaa mawii matatu ambao unakuwepo wa maongezi kidogo basi yanaweza kujibiwa baadhi ya maswali ya papo kwa papo.

Ushauri kwa Mh. Rais na Viongozi Wengine.
Ushauri wangu kwa Mh. rais na viongozi wengine ni kwamba,nawaomba muwe wapenzi wa kutembelea vyombo mbali mbali vya habari, ambavyo kwa sasa si televisheni na magazeti pekee kama ilivyokuwa zama hizo, ambavyo vingine vimekuwa vikitumika kupotosha ukweli wa habari kwa muda mrefu sasa, kwa sasa mnaweza kupitia tovuti,blogu binafsi mbali mbali
zenye habari nyeti kuliko hata ambavyo mnaweza kufikiri. Hizi ni zama za Utandawazi na mambo mengi yako bayana na yataendelea kuwa bayana siku hadi siku kwa maana kila mtu sasa ana uwezo wa kuwa mwanahabari na kurusha habari hewani duniani kote bila ya kutegemea vyombo kama BBC, CNN, Radio Tanzania, TVT ama ITV na vingine vingi na pengine bila hata malipo kama ambavyo nifanyavyo mimi na wanablogu wengine wengi tu duniani. Internet ndiyo kila kitu Zama Hizi za Habari kwani hata nanyi pia mnawezakuwa na blogu zenu binafsi nasi tuwe tunazitembelea! Hii ndiyo Dunia ya sasa!

Kwa habari zaidi na picha za tukio hili tembelea tanzaniaone.net, tanzaniaone.com, tzuk.net na tzuk.com.

Endelea kutembelea blogu hii kusoma barua ya wazi kwa Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete juu ya sakata la Hali Halisi Ya Wanyama Pori huko mbugani.

No comments: