Thursday 1 February 2007

Salamu toka Kilimanjaro!

Je waijua shule ya watoto yatima Amani ilioko mjini Moshi mjini Kilimanjaro?

Hivi karibuni serikali ilitoa tamko la kufuatilia kwa ukaribu na kuyafungia mashirika au watu binafsi wanaotumia migogo ya watoto yatima au wale walioathirika na virusi vya ukimwi kama njia ya kujipatia kula yao.

Inasemekana wajanja wengi bongo sasa wamegundua kama njia hiyo ndiyo deal ya kuvuta fedha na misaada mingine mbalimbali kutoka mashirika mbali mbali na serikali pia ili kujinufaisha wao binafsi pengine na familia zao.

Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba yapo mashirika au watu binafsi ambao kwao wamejioa muhanga kwa hali na mali kusaidia kufa na kupona kuona kwamba watoto wa mitaani ama wale walioathirika kwa virusi vya ukimwi ama kutelekezwa na familia zao wanapata mahitaji yao muhimu kama chakula, malazi na mavazi na hasa UPENDO ambao wameukosa katika familia. Shule ya AMANI yenye makazi yake mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ni moja kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yako mstari wa mbele kabisa kufanikisha hilo.

Pata habari zaidi kupitia tovuti ya shule hii ambayo ni http://amanikids.wamka.ch,