Sunday 11 February 2007

CCM London Chapter/Reading Kikao!

Jana tarehe 10 Februari 2007,wanachama wakereketwa wa CCM wa tawi la CCM London walifanikiwa kufanya kikao chao cha pili ambacho kilikuwa ni matokeo ya kikao kilichofanyika tarehe 13 Jan 2007 Brent Cross- JIJINI London! Kikao hiki kilichohudhuriwa na karibu ya wanachama Arobani(40), karibu asilimia hamsini ya hao wakiwa ni wanachama kutoka Reading, kulikuwapo pia na baadhi ya wanachama kutoka miji ya mbali na karibu kama Nottingham, Bournmouth, Cardiff, Basingstoke na bila kuwasahau wazee wa jiji kuu la London.

Mojawapo ya agenda zilizozungumziwa katika kikao hicho ni ile ya uchaguzi wa wawikilishi watatu kutoka mji wa Reading ambayo ilifanyiwa kazi kidemokrasia na wajumbe Watatu walichaguliwa kwa kura nyingi kuwakilisha CCM "London Chapter" kutoka Reading ni Ndugu Maina Owino, Ndugu John Lusingu na Dada Susan Mzee. Tunawapa pongezi wajumbe hawa ni matumaini ya wana-CCM kwamba watatuwakilisha kikamilifu kutokana na uzoefu wao na kuonekana kubobea katika mambo ya chama.

M/Kiti kamati ya muda ndugu Sharif Maajar alifafanua pia juu ya swala zima la uchaguzi ambao utafanyika muda si mrefu tarehe bado hajipangwa na alisisitiza kuwa nafasi ziko wazi kwa kila mwanachama mwenye sifa kwenda kuchukua fomu kugombea nafasi hizi yaani kuanzia ngazi ya M/kiti wa Tawi hadi ujumbe. Naye mshauri wa maswala ya kisiasa na sheria wa Tawi ndugu Ridhiwani Kikwete alisisitiza kuwa sifa kuu muhimu ni ile ya Uzawa na umri! Alisema kwamba katiba inasema wazi kwamba mwanachama wa CCM ni lazima awe Mtanzania mwenye umri usiopungua miaka kumi na minane(18).
Mjumbe mmoja toka Bournmouth alipenda ufafanuzi zaidi juu ya jina la Tawi, alisema kwamba jina la "TAWI LA CCM LONDON" linaweza kuwa ni kikwazo kidogo kwa maana baadhi ya wanaCCM wengi wameshindwa kuhudhuria kikao hiki ama vikao vilivyopita wakidai kwamba labda tawi hili linawahusu watu wa London pekee, hivyo basi alihoji kwa nini lisiitwe tawi la CCM Uingereza? Swali hili amablo lilionekana kuwa vichwani mwa wengi na kuleta utata,nalo lilipewa ufafanuzi yakinifu kuwa CCM London ni jina tu na kwamba hatuwezi kusema CCM Uingereza kwa maana CCM si chama cha siasa Uingereza kama ilivyo Labour au Conservative, kwa maneno mengine CCM London/Uingereza haiwezi ku-operate kama CCM nchini Tanzania na kwamba jina hili limetumika kama jia la Usajiri kama CCM London Chapter kule Jumba Kubwa (Home Office), naye Katibu Mwenezi ndugu Yahaya Kimwone alitoa ufafanuzi zaidi kwa kutumia mfano ule wa jina "Azimio La Arusha" ya kwamba chimbuko/ufufuo wa CCM Uingereza tamko rasmi lilianzia pale London na licha ya hayo kwa wale walio nje ya Uingereza London ndiyo Uingereza, kama ilivyo kwa nchi nyingi kufahamika kutoka na majina ya miji yake mikuu, ni utamaduni tu! Kwa maana hata unapoongelea Bongoland ukiwa nje ya Tanzania wengi umaanisha Tanzania(as the whole) kama nchi nzima ingawa unapokuwa ndani ya Tanzania Bongo ni Dar-es-salaam! Watu wa Musoma, Moshi, Mbeya husema Bongo wakiimanisha Dar-es-salaam !

Ni mengi mno yaliyoongelewa katika kikao hiki kilichokuwa na mafanikio kilichofanyika katika ukumbi wa www.readingbusinessvenue.com katikati kabisa ya mji wa Reading, kuanzia saa 9 mchana hadi saa 12 jioni. Kama utapenda kujua habari zaidi za CCM ama kujiunga na CCM wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.

CCM wanasema kama, "Kama huwawezi, Jiunge nao, Usishindane Nao"

"NGUVU MPYA, ARI MPYA NA KASI MPYA"

Shukurani ziwaendee waandalizi wa kikao www.goce.co.uk