Monday 12 March 2007

Uhamiaji/Immigration-UK VISA!

Kwa wale wenzangu na mimi ambao tunaendelea kujikita kwa Bibi(Malkia Elizabeti) kwa kujikimu wenyewe na kutegemea kubeba box ama kuishi kiujanja ujanja, hali imeendelea kuwa ngumu kwa sasa!
Ni wazi kwamba kwa mtanzania ama mgeni(foreigner) kutoka nchi zetu za Dunia ya tatu ambaye yuko nchini Uingereza katika miaka hii ya karibuni( "Msomi bila kusoma ama Mkimbizi bila Vita")-according 2 MrII a.k.a SUGU, hali si kama ilivyokuwa miaka 4,5,6,10 iliyopita. serikali ya Bi Mkubwa(Malkia) imeendelea kubana na kuonyesha kuchoshwa na wageni.
Kuna habari kwamba hivi karibuni serikali hii itakuwa inatumia ujumbe wa simu za mkononi sms/txt msg kuwataarifu watu ambao visa zao zinaelekea kwisha ya kwamba wajiandae kuondoka nchini kwa hiari kabla sheria haijachukua mkondo wake. Si hivyo tu bali pia jumbe hizi za sms/txt zitatumwa pia kwa wenye nyumba(Landlords/LandLadies) kuwataarifu kuwa wateja/wapangaji wao muda wa kuishi hapa umekwisha na kwamba Landlord/Landlady atakayekiuka kushirikiana na serikali kuwafichua watu hawa atalipa faini kwa kila kichwa ambayo inaweza kuwa ni zaidi ya ile wanayolipa waajiri walioajiri wafanyakazi bila makaratasi ambayo ni paundi za mwingereza elfu tano(£5,000) zaidi ya milioni kumi(10,000,000/-) fedha za madafu kwa kichwa na zaidi.
Kwa mtaji huu tuendelee kujetemgemea mtiririko wa vijana nyumbani katika miaka 2 ijayo! Swala ni kwamba je, Vijana tumejiandaaje na Wimbi hili?
Wazaramo wanasema, "We kalaga bao miangu na kidonda chako kuku wakidonole"

CRDB BANK ABROAD- TANZANITE ACCOUNT!

Bank ya CRDB imeendelea kuijitangaza kwa kasi ya nguvu ughaibuni kupitia akaunti yake ya Tanzanite. Bank hiyo kwa kuendelea kuwatumia mawakala wake katika miji mbali mbali ya Uingereza hasa mji wa Reading na Jiji la London, imefanikiwa kupata wateja wengi zaidi kutoka United kingdom.
Mwakilishi wa CRDB bank aliyekuwapo nchini Uingereza dada Jenipher Tondi amefanikiwa kuitangaza akaunti hii ya Tanzanite kwa umakini na hivyo kupelekea vijana kwa wazee, wake kwa waume wakitanzania waishio nchini Uingereza kuonyesha kuvutiwa na huduma hiyo na kupelekea wengi wa hao kufungua akaunti hii ya Tanzanite!
Miaka miwili iliyopita benki ya CRDB ilijaribu kujitangaza nchini Uingereza lakini hii huduma ilionekana kuzorota pengine ni kwa ajili watanzania kutokueleweshwa vizuri faida za uwekezaji nchini Tanzania ama ni hali tu ya maendeleo na shinikizo na hali halisi ya maisha Ughaibuni ilivyo katika miaka hii ya karibuni.
Takwimu zinaonyesha kwamba watanzania zaidi ya elfu mbili(2000) waishio ughaibuni sasa wana akaunti ya Tanzanite. Hivi sasa huduma hii inaweza kupatikana pia kwa njia ya Internet, kama kuangalia bank statement, kulipa bills(umeme, maji, n.k) na kwamba money transfer inaweza kufanyikia kupitia baadhi ya benki kubwa za hapa nchini Uingereza kama Lloyds TSB Bank. moja kwa moja kwenye akaunti ya mteja aliye nje ya nchi bila longolongo lolote!
Kwa ufahamu zaidi unaweza kuwasiliana na dada Jenipher Tondi kwa namba +255-22-2117442/ +255-784719420 ama kwa barua pepe tanzanite@crdbbank.com ama tembelea tovuti yao ambayo ni http://www.crdbbank.com ("The Bank That Listens")