Tuesday 19 June 2007

Bongo Inavyoliwa na Wachache!




Soma habari hizi tatu tofauti kutoka vyanzo tofauti jaribu kupata picha kamili!






1)Ni kwamba tuna fedha sana au? (source: darhotwire)




Ghorofa mbili za Benki Kuu ya TZ zilizojengwa kwenye eneo la mita za mraba 40,000 zimelamba mshiko zaidi ya mara nne kama zingejengwa katika miji tajiri kama New York, London
na Tokyo
.Akimwaga takwimu hizo kwa machungu Kiongozi wa kambi ya upinzani na Waziri kivuli Wizara ya Fedha, Hamad Rashid Mohamed alisema kuwa hivi sasa gharama za kujenga mita moja ya mraba katika mataifa tajiri ni dola za Marekani -$2000.Lakini kwa gharama zilizotumika kujenga minara miwili ya BoT (40,000sq m), dola za Marekani -$8000 zilitumika kujenga mita moja ya mraba.Mwaka jana gharama za ujenzi zilitajwa kuwa dola za Marekani mil. $150 lakini kiasi hicho kimeshazidi sana na hivi sasa BoT inaendelea na ujenzi bila ya kutaja gharama halisi zilikofikia.Mh. Mohamed alisema kuwa hadi sasa majengo hayo hayajamalizika ingawaje yalishafunguliwa rasmi na Rais Mstaafu Benny Mkapa wa awamu ya tatu katika kilichoonekana kama kukurupuka.Hiki si kimeo cha kwanza kwani BoT inahusika na kashfa nyingine ya kutoa mshiko kwa kampuni ya Mwananchi Gold Project inayojihusisha na usafishaji wa dhahabu na nyingine ya dhahabu ya Meremeta.Ndani kwa ndani vilevile kuna vimeo vya upotevu wa fedha na hivi sasa wamesakwa wakaguzi kutoka nje ya nchi ili kuichambua Benki hiyo kubaini kiasi kamili kilichoyeyuka.Wakati yote haya yanaendelea nafasi ya Gavana wa Benki hiyo iko poa tu na hakuna anayesema juu ya lolote kama aachie ngazi au .............anyway si kasumba yetu.






2)Umaskini wetu unaletwa na viongozi - Anne Malecela 2007-06-20 08:47:31 Na Boniface Luhanga, Dodoma




Mbunge wa Same Mashariki (CCM), amesema watu waliopewa dhamana ya kuongoza nchi hii ndio wanaoimaliza kwa kuzidi kuitumbukiza katika janga la umaskini. Akiongea kwa uchungu bungeni jana, Mbunge huyo, Bi. Anne Kilango Malecela, aliwakemea vikali baadhi ya viongozi serikalini wenye dhamana ya kusaini mikataba kuwa waaminifu kwa kuweka maslahi na uzalendo mbele na kumuogopa Mungu, vinginevyo watalifikisha taifa mahali pabaya. Hali kadhalika, mbunge huyo amesema hakubaliani hata chembe na hatua ya serikali ya kupitisha moja kwa moja (fast tracking) bila ukaguzi bidhaa zote zinazoingizwa na wafanyabiashara ambao `eti` tayari wameainishwa kama wawajibikaji wazuri katika kulipa kodi. Bi. Malecela alitoa msimamo huo jana alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha (2007/08). Hotuba hiyo iliwasilishwa Bungeni Alhamisi iliyopita na Waziri wa Fedha, Bi. Zakia Meghji. Akielezea suala la mikataba, mbunge huyo alisema, anaamini kwamba Tanzania siyo maskini kiasi hicho lakini kinachochangia kuiangusha, ni mikataba mibovu inayosainiwa na baadhi ya viongozi wenye dhamana hiyo ambao hawazingatii uzalendo na maslahi yaTaifa. Kwa mujibu wa Bi. Malecela, Tanzania ni nchi ya tano barani Afrika kwa utajiri kutokana na kuwa na raslimali nyingi. Hata hivyo, alisema pamoja na hali hiyo, bado Tanzania inaonekana kuwa maskini na kwamba umaskini huu ni wa kujitakia kwani unachangiwa na viongozi wenye ubinafsi. `Kila anayesaini mkataba, amuogope Mwenyezi Mungu? Amtangulize Mungu wake mbele? Nchi hii si maskini kiasi hiki, ni tajiri na yenye raslimali nyingi ambayo inashika nafasi ya tano katika Bara la Afrika,` alisisitiza kwa uchungu. Alisema Rais Jakaya Kikwete, ameonekana kuwa amedhamiria kuitumikia kwa dhati nchi yake na ndio maana amekuwa akisema mara kwa mara kuwa anakerwa sana na umaskini wa Watanzania walio wengi, lakini baadhi ya watendaji, wanataka kumuangusha. Alitolea mfano wa Shirika la Ndege (ATC) ambalo aliwahi kulifanyia kazi, kwamba limefikishwa mahala liliko sasa ambako ni mahututi kutokana na mikataba hiyo isiyoangalia maslahi ya nchi yetu. Alimshauri Rais Kikwete kuwachukulia hatua kali watendaji wa namna hiyo bila kuwaonea huruma. `Ukimwangalia nyani akilia, anatia huruma kuliko hata mjane na ukitaka kumuua nyani anayekula mazao yako shambani, usimwangalie usoni maana utamuone huruma,` alisema akimaanisha kwamba, Rais Kikwete awachukulie hatua kali watendaji wabovu pasipo kuwaonea huruma. Aliwataka watendaji katika ngazi zote Rais Kikwete kutokana na jitihada zake na kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake. Kuhusu hatua ya serikali ya kupitisha moja kwa moja (fast tracking) bila ukaguzi bidhaa zote zinazoingizwa na wafanyabishara ambao tayari wameainishwa kama wawajibikaji wazuri katika kulipa kodi, Bi. Malecela alisema hakubaliani hata kidogo. Alisema anaamini kabisa kuwa kila mfanyabiashara awe mdogo ama mkubwa, hufanya biashara zake kwa kutaka kupata faida kubwa zaidi siku zote. Aliihoji serikali imenguanduaje uaminifu wa wafanyabiashara hao hata ikaamua kufikia hatua hiyo. `Tena mmewachagua wafanyabiashara watakaopitisha bidhaa zao bandarini bila kukaguliwa eti wameonyesha kuwajibika, hivi mmeingia mioyoni mwao lini (na kuona kwamba sasa wao ni sawa na malaika?),` Alihoji na kuongeza kamwe yeye hilo hakubaliani na kuitahadharisha serikali kuwa, hatua hiyo itakuja kuleta hatari kubwa kwa Taifa. `Mimi nasema `No`, tutaimaliza nchi sasa , eti makontena yao yakiingizwa nchini, yanapita bila kukaguliwa? Hapana, hii ni hatari. Serikali inapaswa kuliangalia upya suala hili,` aliongeza Bibi Anne Kilango Malecela ambaye pia ni mfanyabiashara. Naye Bi. Joyce Machimu (CCM-Viti Maalum), aliitahadharisha serikali kuhusu huo mpango wa kutokagua baadhi ya bidhaa za wafanyabiashara, kwa maelezo kuwa, wafanyabiashara wengine wasiokuwa waaminifu, wanaweza kutumia mwanya huo kuingiza mihadarati nchini.
SOURCE: Nipashe






3) nitumie email yako, nikutumie kiambatanisho cha kurasa tisa cha mtandao wa walaji wakuu bongo ambayo ina-link na hizo habari hapo juu.