Wednesday 7 February 2007

Misukosuko ya Bomu La Barua/ Letter Bomb Threat in UK

Miji kadhaa hapa nchini Uingereza imekumbwa na homa ya Bomu la Barua "Letter Bomb Threat". Tayari miji mitatu katika siku tatu mfululizo kumekuwapo na milipuko ya mabomu yaliyotumwa kwenye barua.
Bomu la kwanza lilipuka tarehe 5 Februari 2007 katika kitogoji cha Victoria Jijini London na kumjeruhi mama mmoja. Siku iliyofuata ya tarehe 6 Februari 2007 kukalipuka bombu lingine katika mfumo huo huo wa barua katika kitongoji cha Wokingham- Berkshire, na halafu tarehe 7 Februari 2007 kumekuwapo na mlipuko mwingine tena huko Swansea makao makuu ya ofisi za DVLA kusini mwa nchi ya Uingereza na kumjeruhi mama mmoja.

Polisi wa Uingereza bado wanafanya uchunguzi kujua ni nini hasa asili ya vitisho hivi ambavyo vinaonekana kuunganishwa na jambo fulani. Mabomu saba zaidi yameshagundulika ambayo yamekuwa yakielekezwa kwa watu fulani fulani.

Mfululizo huu wa mabomu unafananishwa na true story fulani iliyowahi kutokea huko marekani miaka ya nyuma, ambapo mtu mmoja aliamua kulipua mabomu ya aina hii kuweka msisitizo juu ya ukatili wa wanyama.

Endelea kutembelea blogu hii kwa habari zaidi

No comments: